Kahama FM

Kahama watakiwa kuwa mabalozi kwa wanawake wajawazito

September 30, 2024, 5:07 pm

mratibu wa elimu ya afya kwa umma manispaa ya Kahama Asteria Kamanga,[picha na Kitila Peter]

Wananchi wanapaswa kutumia huduma M-MAMA ili kuendelea kupunguza vifo vya mama na mtoto wakati wa kijifungua, huku wenza wao wanatakiwa kufahamu afya mama mjamzito ili inapotokea changamoto wanalitatua mapema.

Na Leokadia Andrew

Wananchi wa Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kuwa mabalozi kwa wanawake  wajawazito wanapowaona wana dalili za hatari wawahishe hospitali mapema ili kuondokana na vifo vya mama na mtoto wakati wa kijifungua.

Kauli hiyo imetolewa leo na mratibu wa elimu ya afya kwa umma manispaa ya Kahama Asteria Kamanga, wakati akizungumza na Kahama fm, ambapo ameitaka jamii kuwasisitiza kula vyakula vya makundi matano ya vyakula ili kuongeza damu.

Sauti ya mratibu

Kwa upande wake, Mratibu wa usafiri wa dharura kwa wajawazito na watoto wachanga manispaa ya Kahama (M-MAMA PROGRAM) Anesius Rweikiza amesema wananchi wanapaswa kutumia huduma M-MAMA ili kuendelea kupunguza vifo vya mama na mtoto wakati wa kijifungwa, huku akiwataka wenza wao kufahamu afya mama mjamzito ili inapotokea changamoto wanalitatua mapema.

sauti ya Anesius Rweikiza

Taarifa kutoka taasisi ya Tanzania Demographic Eath Surviy, imesema vifo vya mama na mtoto vimepungua ambapo miaka ya nyuma kulikuwa na vifo zaidi ya 500 katika vizazi hai 100,000, huku kwa sasa ripoti inaonyesha vimepungua na kufikia 104.