Kahama FM
Kahama FM
March 23, 2026, 6:18 pm

Na Sebastian Mnakaya
Zaidi ya mabinti 18 wanaoishi katika mazingira magumu halmashauri ya Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga, wamepatiwa ufadhili na serikali kusomeshwa katika elimu ya ufundi VETA kwa fani mbalimbali, ikiwemo ufundi cherehani na ususi.
Akizungumza wakati wa kuwaaga mabinti hao kuelekea chuoni, Afisa ustawi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama Swahiba Shemshem, amesema serikali kwa kushirikia na shirika WiLDAF katika mradi wa Chaguo langu Haki yangu, wameendelea kuwafadhili mabinti hayo, waliokatishwa masomo kutokana na sababu mbalimbali.
Aidha, Swhiba amesema kuwa baada ya kumaliza kozi hizo watapatiwa vitendea kazi ili waweze kujiajiri wao wenyewe, huku akiwataka wazazi kuacha tabia ya kuwaozesha watoto wao wakiwa na umri mdogo na badala yake waache wasome ili watimize ndoto zao za baadae.

Kwa upand wao, baadhi ya mabinti hao wakizungumza kwa nyakati tofauti, akiwemo Hawa Selemani Abduli, Tedy Boniphas na Esther John, wameishukuru serikali kwa kuwapatia ufadhili wa masomo hayo ambayo yatawasaidia katika maisha yao ya baadae.
Hata hivyo, mpaka sasa zaidi ya mabinti 261waliokatishwa ndoto zao kwa sababu mbalimbali walipatiwa ufadhili huo ambao kila moja kwa sasa anaendelea na shuguli zake.