Kahama FM

Wanawake Kahama mguu sawa tuzo za ‘mwanamke mjasiriamali’

March 20, 2026, 9:18 pm

Katika Uzinduzi wa Mwanamke Mjasiliamali (Picha na Dauda DHD)

”Wajasiriamali wa wilaya ya Kahama, changamkieni fursa kupitia jukwaa la Mwanamke Mjasiriamali”

Sebastian Mnakaya

Wanawake wajasiriamali wilayani Kahama mkoani Shinyanga wamezindua jukwaa lao la Mwanamke Mjasiriamali kwa lengo la kusaidiana katika shughuli zao za kujipatia vipato pamoja na mikopo isiyokuwa na masharti magumu.

Kiongozi wa jukwaa hilo Salome Mvanga akizungumza wakati wa uzinduzi wa jukwaa hilo ulifoanyika katika Manispaa ya Kahama, ambapo amesema kuwa lengo la kuwa na jukwaa hilo ni kuwezeshana wanawake kiuchumi na kuinuana katika biashara.

Salome Mvanga akizungumza na wanawake wafanyabiashara mbalimbali katika mji wa Kahama

Aidha, Mvanga amesema kuwa wanatarajia kuanzisha tamasha la MWANAMKE MJASILIAMALI ambalo linatarajiwa kufanyika mei mosi mwaka huu 2026, litakalo husisha wajasiliamali mbalimbali wanofanya shughuli zao katika mijini wa Kahama, ikiambana na tuzo mbalimbali.

Sauti ya Kiongozi wa jukwaa la Mwanamke Mjasiliamali Salome Mvanga

Mvanga ameongeza kuwa ili wakina mama wajasiliamali wafanikiwe zaidi wanapaswa kushirikiana na kuwa wamoja katika shughuli zao, huku akiwataka kuchangamikia fursa ya kushiriki katika tuzo zinazoandaliwa na Mwanamke Mjasiriamali.

Sauti ya Kiongozi wa jukwaa la Mwanamke Mjasiliamali Salome Mvanga

Kwa upande wao, baadhi ya wajasiliamali akimwemo Grace Zagamba na Delmas Mathias, wamesema kuwa jukaa hilo litawasaidia wakina mama kuinua, kuzionesha na kuziendeleza biashara zao pamoja na kupata mikopo nafuu kupitia jukwaa hilo.

Sauti ya wajasiriamali akimwemo Grace Zagamba na Delmas Mathias

Hata hivyo, jukwaa hilo linatarajia kuanzisha tuzo mbalimbali za MWANAMKE MJASILIAMALI kwa wilaya ya Kahama, ikiwalenga wanawake wajasilimali katika kuwainua.