Kahama FM

TANESCO Kahama pelekeni huduma ya umeme kwenye mitaa ya shunu na mtakuja

February 22, 2026, 1:16 pm

Diwani wa kata ya Nyahanga Josephine Kilimba wakati akizungumza katika kikao na shirika la umeme Tanzania (TANESCO)

”wananchi wanahitaji huduma ya umeme kwenye maeneo ambayo mpaka sasa hajafikiwa, ikiwa miundombinu imefika kwenye maeneo hayo”

Wananchi wa mtaa wa Shunu na Mtakuja katika kata ya Nyahanga halmashauri ya Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga wameliomba shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kupatiwa nishati ya umeme katika baadhi ya maeneo ambayo mpaka sasa hajapata huduma hiyo.

Kauli hiyo imetolewa na diwani wa kata ya Nyahanga Josphine Kilimba, wakati wa kikao kati ya TANESCO na madiwani wa manispaa ya Kahama kilicholenga kujadili miradi mbalimbali ya umeme katika mitaa na vijiji pamoja na namna bora kulinda miundombinu ya umeme.

Aidha, Kilimba amesema kuwa kuna baadhi ya maeneo mpaka sasa hayajapatiwa umeme katika kata hiyo, ikiwemo shunu mlimani, kaudo kaskazini, mji mwema, huku akiomba kuangalia maeneo muhimu kama taasisi kupatiwa umeme ili shughuli za kimaendeleo ziendelee.

Sauti ya diwani wa kata ya Nyahanga Josephine Kilimba

Kwa upande wake, Mhandisi Mwandamizi wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO Mkoa wa Shinyanga Anthony Tarimo, akitoa ufafanuzi juu ya changamoto ya umeme kwa maeneo ambayo hayajafikiwa, amesema kuwa watayashugulikia maeneo hayo ili yapate huduma hiyo, ikiwa miundombinu ya umeme tayari imefika katika maeneo hayo.

Sauti ya Mhandisi Mwandamizi wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO Mkoa wa Shinyanga Anthony Tarimo

Hata hivyo, katika vitongoji 61 Manispaa ya Kahama vinatarajiwa kunufaika na huduma ya Umeme kupitia Mradi unaotekelezwa na Wakala wa Nishati ya Umeme Vijiji REA chini ya Usimamizi wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO.