Kahama FM

Mfumo wa IDRAS kupunguza gharama kwa wafanyabiashara

February 3, 2026, 9:54 am

Wafanyabiashara wilayani Kahama wakiwa kwenye mafunzo ya mfumo mpya IDRAS

Mfumo wa ADRAS utawasaidia wafanyabiashara kupunguza gharama kwa kufuata huduma katika ofisi za TRA badala yake wataweza kuipata popote pale walipo”

Baadhi ya wafanyabiashara ya Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, wamesema kuwa kuanza kwa kutumika mfumo Integrated Domestic Revenue Administration System (IDRAS), utawapunguzia gharama za kufuata huduma katika ofisi za Mamlaka ya Mpato Tanzania TRA pamoja na kulipa kodi kwa wakati.

Hayo yamesemwa na baadhi ya wafanyabiasha, akiwemo Chona Mchunga na Nassoro Maige, wakati wakipatiwa mafunzo ya namna ya kutumia mfumo huo, yaliofanyika wilayani Kahama, ambapo wamesema kuanza kutumika kwa mfumo utawasaidia kufahamu mwendeo wa ulipajiwa mapato kwa wakati.

Sauti mbalimbali za wafanyabiashara wa wilayani Kahama

Akifungua mafunzo hayo, kaimu meneja wa TRA Kahama Isack Mgongolwa amesema kuwa IDRAS Ni mfumo mpya utakaojumisha mifumo yote inayosimamiwa na TRA, ambayo itawasaidia wafanyabiashara kujua huduma mbalimbali kupitia mfumo.

Sauti ya kaimu meneja wa TRA Kahama Isack Mgongolwa

Afisa msimamizi wa kodi, idara ya elimu na mawasiliona mkoa wa kikodi kahama (TRA) Hamisi Sanze, amesema kuwa baada ya mafunzo hayo na mfumo kuanza, itawarahisishia wafanyabiasha kupata hudama zote kupitia IDRASpamoja na kupata taarifa za ulipaji wa kodi kwa wakati.

Sauti ya Afisa msimamizi wa kodi, idara ya elimu na mawasiliona mkoa wa kikodi kahama (TRA) Hamisi Sanze

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inatarajia kuanza kutumia mfumo Integrated Domestic Revenue Administration System (IDRAS), kuanzia febuari 9, 2026.