Kahama FM
Kahama FM
February 3, 2026, 9:32 am

”Kwa mwaka 2025, mahakama za mwanzo za wilaya ya Kahama zimefanikiwa kumaliza kesi zote na kuvuka kesi”
Mahakama za mwanzo wilayani Kahama mkoani Shinyanga kwa mwaka 2025 zimefanikiwa kumaliza kesi zote kwa mwaka huo na kuvuka na kesi 0.
Hayo yamesemwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Kahama Edmund Kente, wakati wa uzinduzi wa wiki ya sheria nchini inayoashiria kuanza rasmi kwa shughuli za mahakama.
Kente amesema kuwa kuendelea kutoa haki kwa wateja wao kwa kasi kama hiyo ya utekelezaji kwa mwaka 2025 ili kumaliza kesi kwa wakati ili wananchi wapate haki yao pasipokupoteza muda wakati wa uendeshaji wa kesi.

Naye, Mwakilishi wa mkuu wa Wilaya ya Kahama TUmshukuru Mdui, amesema mahakama inao wajibu wa kutoa haki na si kuwahishwa kwa kutolewa hukumu tu bali kuzingatia utoaji wa haki.
Akitoa hotuba katika maadhimisho hayo Wakili wa Serikali kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Satuninus Kamala amesema maadhimisho hayo yanaashiria kuanza rasmi kwa shughuli za mahakama akisema kuwa Mapendekezo mengi ya Tume ya Haki Jinai ya mwaka 2023 yameanza kutekelezwa.
