Kahama FM

Vijana Malunga watakiwa kujiari wao wenyewe

January 27, 2026, 1:54 am

Vijana wa kata ya Malunga wilayani Kahama wakabidhiwa cherehani 4 na mashine 1 na diwani wa kata ya Malunga Ahamed Harun( Picha na Sebastian Mnakaya)

Na Sebastian Mnakaya

Vijana wa kata ya Malunga wilayani Kahama mkoani Shinyanga wamekabidhiwa Cherehani 4 na Mashine ya kuchomelea 1, vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 1.9 ili kujiari na kujikwamua kiuchumi.

Akikabidhi vifaa hivyo mbele ya mkutano wa hadhara ulifanyika katika viwanja vya soko la Malunga, ambapo diwani wa kata hiyo, Ahamdi Haruna amesema kuwa ametoa vifaa hivyo kwa ajiri ya vijana kuanza kujiali wao wenye na wasitegemee kuajiliwa pekee.

Aidha, Ahamdi amesema kuwa kwa sasa ajira zimekuwa ngumu na kuwaomba vijana wengi kutumia fursa zilizoopo kujiari wenyewe na wasisubili ajira kutoka serikali ili waweze kutengeneza uchumi kupitia kujiajiri.

Sauti ya diwani wa kata ya Malunga Ahamdi Harun

Nae, wenyekiti wa vijana wa chama cha mapinduzi (CCM) kata ya Malunga, David Kagoma amemshukuru diwani wa kata hiyo kwa kuwapatiwa mashine hizo ili waweze kujiajiri wao wenyewe, huku akiomba serikali kuwatizama kwa jicho la tatu katika suala zima la ajira ili waweze kuongeza vipato vyao.

Sauti ya wenyekiti wa vijana wa chama cha mapinduzi (CCM) kata ya Malunga, David Kagoma
Mkutano wa hadhara ukiendelea