Kahama FM
Kahama FM
January 10, 2026, 1:41 pm

Na Sebastian Mnakaya
Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) wilayani Kahama Mkoani Shinyanga, wametakiwa kuwasimamia vizuri wakandarasi ili waweze kujenga barabara zenye ubora pamoja na kuzimaliza kwa wakati ili njia barabara zipitike wilayani humo.
Wito huo umetolewa na Mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini, Benjamin Ngayiwa, wakati alipofanya ziara ya kukagua barabara za kahama katika kipindiki cha mvua, ambapo amesema kuwa moja kero ya wananchi wa Kahama ni ubovu wa barabara.
Aidha, amemtaka meneja wa TARURA wilaya ya kahama yeye pamoja na timu yake uendelea kuwasimamia vyema wakandarasi kumaliza miradi ya utengenezaji wa barabara kwa wakati na kwa mujibu wa mikataba ili njia zifunguke na kupita.

Kwa upande wake kaimu meneja wa TARURA wilaya Kahama, Mhandisi Masolwa Juma amewataka wakandarasi kuendelea kutekeleza miradi kwa wakati, huku akiishukuru serikali kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili miradi ya ujenzi wa barabara za lami, ambapo kwa kahama wanatarajia kujenga kilometa 12 za rami.

Awali, mkandarasi anayetekeleza baadhi ya barabara za jimbo hilo Mhandisi Paul Maila amewaahidi wananchi wa mtaa wa mtakuja, kuanza kutekelezaji mradi huo wa uufunguaji wa njia za barabara katika eneo ili ianze kupitika.
Mbunge wa jimbo la Kahama mjini Benjami Ngayiwa ameanza ziara zake za kusikiliza na kutatua kero za wananchi, huku akianzia katika kukagua barabara zote za jimbo la Kahama mjini.

