Kahama FM
Kahama FM
August 19, 2025, 12:26 pm

”watembea kwa miguu zingatieni upande wao sahihi wa kupita, kwa mjibu wa sheria za usalama barabarani ni mkono wa kulia wa mtumiaji ili kutoa nafasi ya kuona chombo cha moto kilichombele yake”
Na John Juma
Watumiaji wa barabara katika Halmashauri ya Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kuzingatia kanuni, taratibu na sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali zisizo za lazima pamoja na kuondokana na adhabu.
Hayo yamesemwa na Mrakibu wa Polisi na Mkuu wa Usalama Barabarani wilayani Kahama Flora Nangawe wakati akizungumza na Kahama fm ofisini kwake, ambapo amesema madereva na watembea kwa miguu wanapswa kuzifahamu sheria za usalama barabarani kwa usalama wao.
Nangawe amewataka watembea kwa miguu kuzingatia upande wao sahihi wa kupita ambao kwa mjibu wa sheria za usalama barabarani ni mkono wa kulia wa mtumiaji ili kutoa nafasi ya kuona chombo cha moto kilichombele yake.
Nao, Watumiaji wa barabara wakizungumza kwa nyakati tofauti tofauti akiwemo, Marium Emmanuel, Remidius Kaijage na Malaki Firmoni wamezitaka mamlaka kuweza kuborehsa miundo mbinu pamoja na kutoa elimu juu ya usalama barabarani.

Kwa upande wao madereva wa vyombo vya moto akiwemo Yossam Abdallah na Krivin James wameiomba serikali kuboresha miundombinu ili kuwe na njia ya watembea kwa miguu ili kuondokana na ajali za mara kwa mara.
Barabara ni moja kati ya miundombinu muhimu inayokuza uchumi wa nchi yetu na kuchangia ukuaji wa Taifa kwa kiasi kikubwa kwa kupanua biashara ya ndani na kimataifa kwa njia ya usafirishaji.
