Kahama FM
Kahama FM
August 9, 2025, 8:32 pm

Tanzania Commercial Banki (TCB) kwa mwaka jana imetoa mikopo zaidi ya shilingi bilioni 360 kwa wabiashara wadogo na wakati kwa vigezo rafiki.
Na Sebastian Mnakaya
Wananchi wilayani Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kuachana na mikopo kwenye taasisi za kifedha zisizo rasmi ili kuondokana na changamoto za kukapoa mikopo umiza yenye riba kubwa na isiyokuwa na tija.
Hayo yemesemwa na Afisa mtendaji mkuu na mkurugenzi mtendaji wa benki ya Tanzania Commercial Banki (TCB) Adam Mihayo katika hafla iliyowakutanisha na wafanyabiashara wa Kahama, ambapo amesema mpango mkakati wa benki hiyo ni kuwasaidia wafanyabiashara wadogo na wakati ili kuwainua kiuchumi katika biashara zao.

Aidha, Mihayo amesema kuwa kwa mwaka huu benki hiyo imeweza kutengeneza faida ya shilingi bilioni 30 kabla ya kodi, huku wakijikita zaidi katika kuhudumia katika sekta za kilimo na ufugaji, madini na biashara.
Baadhi ya wafanyabiashara na wajasilimali wilayani Kahama, akiwemo Asha Husseni ameishuru benki ya TCB kwa kutoa mikopo isiyokuwa na riba kubwa na masharti magumu, huku Lazaro Kasono akiipongeza benki hiyo kwa kutoa mikopo kwa wakulima ambayo imewasaidia kulima kilimo bora na chenye tija.

Tanzania Commercial Banki (TCB) kwa mwaka jana imetoa mikopo zaidi ya shilingi bilioni 360 kwa biashara wadogo na wakati kwa vigezo rafiki.