Kahama FM
Kahama FM
July 10, 2025, 5:17 pm

”kasikilizeni na kuzitatua changamoto mbalimbali za wananchi wenu pamoja na kushirikiana katika suala ya maendeleo” Mboni Mhita
Na Sebastian Mnakaya
Viongozi wa wilayani ya Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kuendelea kusikiliza na kutatua changamoto mbali mbali za wananchi wao pamoja na ukamilishaji wa miradi ya maendeleo.
Agizo hilo limetolewa na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita wakati wa hafla ya kukabidhiana ofisi ya mkuu wa wilaya ya Kahama Frank Nkinda, ambapo amemtaka kushirikiana na wananchi katika shughuli za maendeleo, huku wakikamilisha miradi hiyo kwa mapato ya ndani.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Kahama Thomasi Muyonga, amemtaka mkuu wa wilaya huyo, Frank Nkinda kuendelea kutekeleza shughuli za kimaendeleo baada mtangulizi wake kuwa mkuu mkoa wa Shinyanga.

Nae, mkuu wa wilaya ya Kahama Frank Nkinda wakati akikabidhiwa ofisi hiyo, amesema kuwa amepokea maagizo hayo na atayasimamai vyema kwa kushirikiana na wananchi katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo.
Wilaya ya Kahama ina jumla ya halmashauri tatu akiwemo Manispaa ya Kaham, Halmashauri ya Ushetu na Msalala, ikiwa na jumla ya mitaa 35, vijiji 146 na vitongoji 1,150.