Kahama FM

Zaidi ya wanachama 100 CCM Shinyanga wachukua fomu kwa nafasi mbalimbali

July 4, 2025, 5:51 pm

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa(Picha Maktaba)

”Mgombea yeyote aliyechukua na kurejesha fomu endapo ataendelea kufanya mambo nje ya utaratibu kwa kukushanya watu hususan wale wajumbe watakaoshiriki kura za maoni atakuwa amekiuka kanuni” Mlolwa

Na Sebastian Mnakaya

Zaidi ya wanachama 100 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Shinyanga wamejitokeza kuchukua fomu za kuwania viti vya Udiwani na Ubunge.

Akizungumza na Kahama fm kwa njia ya simu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa amesema muitikio wa wanachama kuchukua fomu za kuwania nafasi za udiwani na Ubunge ni mkubwa ikilinganishwa na awamu iliyopita.

Aidha, amesema kuwa kwa nafasi ya Ubunge ni zaidi ya Wanachama mia moja wamejitokeza kuchukua fomu katika kugombea nafasi mbalimbali katika chama hicho.

Sauti ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa

Mlolwa amesema mgombea yeyote aliyechukua na kurejesha fomu endapo ataendelea kufanya mambo nje ya utaratibu kwa kukushanya watu hususan wale wajumbe watakaoshiriki kura za maoni atakuwa amekiuka kanuni na atakuwa amejiengua kwenye mchakato huo.

Sauti ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa