Kahama FM
Kahama FM
July 1, 2025, 10:34 pm

Kupitia mradi wa Mpango Kabambe Kidikitali, Kahama kuwa mji wa kisasa ifikapo 2050
Na Sebastian Mnakaya
Baadhi ya Migogoro ya ardhi katika Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga inakwenda kufikia mwisho baada ya kuanza kwa mradi wa Mpango Kabambe wa kidikitali (Muster Plan) utakaotekelezwa mpaka mwaka 2050 ili kufanya Kahama kuwa mji wa kisasa na ulipangika.
Hayo yamesemwa na Mtaalam mshauri kutoka Kampuni ya Urban Solution. (ICE Expert) Hamisi Mkoma wakati wa mafunzo kwa watendaji wa vijiji, kata na wenyeviti wa vijiji wa Manipaa ya Kahama ili kuanza kutekeleza mradi huo, ambapo amesema kwa kata 8 za vijiji zitabadilika katika sekta mbalimbali ikiwemo masuala ya ardhi, Mazingira, biashara na kilimo na mifugo.
Aidha, Mkoma amesema kuwa baada ya kukamili kwa mradi huo Kahama itakuwa mji wa kisasa na wenye mpangilio mzuri hali itakayosababisha halmashauri nyingine nchini kuja na kujifunza ikiwa ni kwa mara ya kwanza kufanyika katika Manipaa ya Kahama.

Kwa upande wao, Afisa mtendaji wa kata ya Kilago Cosmas Bukango na afisa mtendaji wa kijiji cha Isagehe Amina Mgumba wamesema kuwa Mpango huo utasaidia kuondoa utapeli kwa baadhi ya watu wanoazisha migogoro ya ardhi kwa kuwa na mifumo ya kidikitali itakayorahishia kuondoa migogoro hiyo.

Baadhi ya wenyeviti wa vijiji wa Manispaa hiyo, akiwemo mwenyekiti wa kijiji cha Sangilwa Abdala Kingi amesema kuwa kwa kuanza mradi huo utapunguza migogoro ardhi, huku mwenyekiti wa kijiji cha Nyandekwa Shadrack Daud akiomba serikali kushirikiana na wataalum kuendelea kutoa elimu juu ya badiliko katika sheria kabla ya kuanza kwa utekelezaji wa mradi huo.

Mradi huo unakwenda kutekelezwa katika kata 20 za Manispaa ya kahama, huku kata za kinaga, Isage, Mondo, Ngogwa, Nyandekwa, Kilago na Wendele zinakwenda kubadilika kutoka kwenye vijiji na vitongoji kuwa mitaa.