Kahama FM
Kahama FM
June 12, 2025, 2:46 pm

”Wananchi acheni tabia ya kukata miti hovyo ili kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi”
Na Sebastian Mnakaya
Wananchi wa kijiji cha Chela katika halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kuendelea kutunza na kulinda mazingira katika maeneo yao, na kutokufanya shughuli za kibinadamu za ukatiji miti
Agizo hilo limetolewa na mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita wakati wa mkutano wa kusikiliza kero za wananchi ofisini kwake, ambapo amesema kwa baadhi wa wananchi waliokamatwa kutokana na uharibifu wa mazingira na kuchukuliwa vitu vyao warejeshewe.
Aidha Mhita amewataka serikali ya kijiji na kata kuzingatia sheria, kanuni na taratibu katika ukamataji wa wananchi wanaoharibu mazingira, huku akiwataka wananchi kuacha tabia ya kukata miti hovyo ili kuondokana na mabadiliko ya tabia nchi.
Awali, mkazi wa kijiji cha Chela Gabriel Venance amesema kuwa utaratibu uliotumika kuwakamata haukuwa sahihi, huku mtendaji wa kijiji hicho Juma Said akisema watu hao walikamatwa na walipatiwa dhamana na kutozwa faini kutokana na ukataji wa mkaa katika kijiji hicho.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha chela Marco Mayala amesema kuwa waliitisha mkutano wa kijiji kwa ajili ya kutoa tangazo la kutoendelea kufanya shughuli za ukataji wa miti kwa ajili ya mkaa ili kuutunza mazingira