Kahama FM
Kahama FM
May 31, 2025, 3:21 pm

Serikali wilayani Kahama imewapongeza na kuwashukuru shirika la suluhisho la wanawake na vijana (Wayds) kwa kuandaa na kuratibu kongamano la afya ya akili.
Na Sebastian Mnakaya
Serikali wilayani Kahama imewapongeza na kuwashukuru shirika la suluhisho la wanawake na vijana (wayds) kwa kuandaa na kuratibu kongamano la afya ya akili lililofanyika wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Pongezi hizo zimetolewa na mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita ambaye alikuwa mgeni rasmi wa kongamano hilo kwa niaba ya Waziri wa afya Jenista Mhagama.

Sambamba na hayo Mhita amepongeza na kushukuru hatua ya serikali ya awamu ya sita kujenga kituo cha waraibu wa dawa za kulevya Kahama hali itakayowasaidia vijana waliothirika kupata elimu na kutunzwa katika kituo hicho.
Kwa upande wake mkurugenzi wa shirika la maendeleo kwa wanawake na vijana (WAYDS) Charles Deogratius amesema kuwa kupitia mkutano huo wa afya ya akili wanaanzisha mwamko mpya wa kitaifa ili kutatua tatizo la afya ya akili.
