Kahama FM

Viongozi wa chama cha msingi wabainika kugawana fedha za wakulima

May 28, 2025, 3:44 pm

Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga, Donasian Kessy akizungumza na waandishi wa habari

Miongoni mwa waliopokea fedha hizo ni Bi. Lucy Masanja Gidabita, mke wa Katibu Meneja, ambaye alipokea shilingi milioni 34.58, pamoja na Bw. Charles Charles Masanja aliyelipwa shilingi milioni 5.58.

Na Estomine Henry.

Viongozi wa chama cha msingi Ibambala Halmashauri ya ushetu, wilayani kahama mkoani Shinyanga  wamebainika kugawana fedha za wakulima kiasi cha shilingi milioni 151.53 zilizotolewa na kampuni ya Alliance One kama fidia kwa wakulima wa zao la tumbaku waliopata hasara kutokana na mafuriko yaliyotoekea katika msimu wa kilimo wa mwaka 2023/2024 na kusababisha hasara.

Hayo yameelezwa leo na Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Shinyanga, Donasian Kessy wakati akiwasilisha taarifa ya robo ya tatu ya kipindi cha januari hadi machi kwa mwaka 2024/2025 kupitia vyombo vya habari.

sauti ya mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Donasian Kessy

Kessy amesema TAKUKURU ilibaini kuwa shilingi milioni 11.62 zilichukuliwa na baadhi ya viongozi wa chama hicho kwa matumizi yao binafsi, akiwemo Katibu Meneja Bw. Charles Alex Shiyengo na Mwenyekiti Bi. Faida Paulo Deva

Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU mkoa wa Shinyanga, Donasian Kessy

TAKUKURU pia imeweza kutoa wa elimu kwa umma kwa kuendesha imeendesha mikutano ya hadhara 61, semina 30, na vipindi vya redio na runinga 13 kupitia programu yao ya Takukuru Rafiki, lengo likiwa ni kuwahamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya rushwa.