Kahama FM
Kahama FM
May 13, 2025, 5:03 pm

”Madawati hayo waliyoyakabidhi ni sehemu ya utaratibu wao wa kurejesha kwa jamii”
Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania wilayani Kahama mkoani Shinyanga wametoa madawati 100 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 9 kwa shule za msingi Wendele na Igwamanoni.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mboni Mhita, ambaye ni mgeni rasmi katika hafla ya kukabidhi madawati hayo kwa shule mbili za Msingi za Wendele iliyopo Manispaa ya Kahama na Igwamanoni iliyopo katika Halmashauri ya Ushetu.

Aidha, Mhita amewapongeza TFS kwa kuendelea kushirikiana na Serikali za Vijiji na Kata zinazoyazunguka maeneo wanayoyasimamia kwa kudumisha ushirikiano na kuwapatia wananchi uelewa juu ya umuhimu wa misitu.

Kwa upande wake, Meneja wa TFS Wilaya ya Kahama Ester Msekwa amesema madawati hayo waliyoyakabidhi ni sehemu ya utaratibu wao wa kurejesha kwa jamii, huku Mkuu wa Shule hiyo akisema kwa kiasi kikubwa msaada huo umetatua changamoto ya upungufu wa madawati katika shule hiyo.
Nao, baadhi ya wazazi wa shule ya Msingi Wendele wakizungumza kwa nyakati tofauti wameipongeza TFS kwa kutoa msaada huo kwa kupunguza changamoto ya upungufu wa madawati, huku mwanafunzi wa shule hiyo Abeli Mathias ameomba kuongezwa kwa walimu katika shule hiyo.
