Kahama FM
Kahama FM
May 6, 2025, 3:28 pm

”amewataka Viongozi chama hicho kwa ngazi zote kutoendekeza Migogoro isiyokuwa na tija katika kipindi hichi cha kuelekea katika Uchaguzi Mkuu”
Na Sebastian Mnakaya
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Mohamed Ali Kawaida amekea Makundi ndani ya Chama hicho Wakati huu wa kuelekea katika Uchanguzi Mkuu wa Mwaka 2025 na kuwataka Viongozi wa CCM mkoa wa Shinyanga kushughulikia suala hilo kwa haraka.
Kawaida ametoa kauli hiyo Katika Mkutano wa Hadhara wa uliofanyika katika Kata ya Bugarama Wilayani Kahama mkoani Shinyanga na kuhudhuriwa na wanachama wa CCM ambapo amewataka Viongozi chama hicho kwa ngazi zote kutoendekeza Migogoro isiyokuwa na tija katika kipindi hichi cha kuelekea katika Uchaguzi Mkuu.
Aidha, Kawaida amewataka viongozi wa chama hicho na wanachama kuendelea kuwa wamoja katika kuelekea uchaguzi mkuu bila ya kugawanyika pamoja na kutatua changamo mbalimbali zinazowakabili.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kahama Thomas Muyonga ameahidi kusimamia Maagizo ya Chama huku Mbunge wa Jimbo la Msalala Idd Kassim Idd akitaja utekelezaji wa Ilani ya Chama hicho.