Kahama FM

Utaratibu wa kumpeleka mbunge Idd kwenye kamati ya maadili haujafuatwa

May 3, 2025, 3:43 pm

diwani wa kata ya Mwalugulu Flora Sagasaga (Picha na Sebastian Mnakaya)

”Kanuni taratibu za kumpeleke kwenye kamati za maadili hazikufuatwa badala yake ni batili”

Na sebastian Mnakaya

Baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga wamesema taratibu zilizotumika kumpeleka kwenye kamati ya maadili Mbunge wa Jimbo hilo Idd Kassim zimekiukwa na kuwa uamuzi huo ni batili.

Hayo yamesemwa na diwani wa kata ya Mwalugulu Flora Sagasaga wakati akizungumza na waandishi wa Habari, ambapo amesema kuwa azimio hilo lililopitishwa na baadhi ya Madiwani halikufuata kanuni za Halmashauri za uendeshaji wa vikao vya Baraza la Madiwani.

Aidha, Sagasaga ameseme katika ajenda za kikao cha baraza la madiwani ya tarehe 30/04/2025 hak na badala ya imeibuka kwenye kikao hicho, ambapo kwenye kikao cha kokasi cha chama cha utekelezaji wa Ilani halikuzungwa iweje kwenye kikao hicho lizungumziwe.

Sauti ya diwani wa kata ya Mwalugulu Flora Sagasaga

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Busangi Alexander Mihayo, wamewataka madiwani wanaotaka kuchukua hatua Mbunge wao kufuata taratibu za kisheria na sio kukiuka kanuni kama ilivyo sasa.

Sauti ya Diwani wa Kata ya Busangi Alexander Mihayo
Diwani wa Kata ya Busangi Alexander Mihayo

Nae, diwani wa Kata ya Ngaya Kisusi Ilindilo amesema kuwa tangu mbunge Idd aingie madaraka wamezeza kutekeleza mirasi mbalimbali ya maendeleo katika jimbo la msasa, huku diwani viti maalum Pili Izengo akichukizwa na uamuzi huo wa baadhi ya madiwani kumjadili mbunge huo kwenye kikao cha baraza za madiwani.

Sauti ya diwani wa Kata ya Ngaya Kisusi Ilindilo na diwani viti maalum Pili Izengo

Haya yanajiri siku chache zimepita tangu baadhi ya Madiwani wakati wa kikao chao cha kawaida kulitaka Baraza hilo kumfikisha kwenye Kamati ya Maadili Mbunge Idd Kassim kwa madai ya kutokuhudhuria vikao na kuwadhalilisha Madiwani hao wakati wa mikutano ya hadhara na wananchi,tuhuma zilizokanushwa na Madiwani waliozungumza leo.