Kahama FM
Kahama FM
May 3, 2025, 1:49 pm

”Wananchi tuache tabia ya kuhusisha magonjwa ya hospitali kwa imani za kishirikina”
Na Sebastian Mnakaya
Wananchi wilayani Kahama Mkoani Shinyanga wametakiwa kutohusishwa ugonjwa wa Polio na imani za kishirikia na badala yake washiriki kikamilifu katika zoezi la kupata chanjo ya ugonjwa huo ili kujikinga.
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita katika kikao cha kamati ya afya msingi wilaya iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali na kidini, ambapo amesema kuwa wanajamii wanapaswa kuondokana na imanai potofu ili kila moja aweze kupata chanjo hiyo.

Nao, baadhi ya viongzi wa dini wilayani Kahama akiwemo katibu wa shehe wa wilaya Husseni Maguruki na mwakilishi wa madhehebu ya kikristo halmashauri ya Msalala Elias Kulwa wamesema chanjo hiyo ni muhimu wanakakiwa kuitumia, huku wakiomba serikali kutoa elimu ili kuondokana na upotoshaji ugonjwa huo kuhusishwa na imani za kishirikina.
Kwa upand wake, mratibu wa chanjo kutoka halmashauri ya Ushetu Saulo Mkama amesema ugonjwa huo huambukizwa na virusi vya polio na unawapata watu wa rika zote, huku akileeza dalili za ugonjwa huo pamoja na namna ya kijikinga.
Hata hivyo, ugonjwa wa Polio umekuwa tishio kwa miaka mingi katika nchi nyingi dunian ikiwemo Tanzania.
