Kahama FM

Baraza la madiwani Msalala limeazimia mbunge wao kuitwa kwenye kamati ya maadili

May 3, 2025, 1:11 pm

Baraza la madiwani likiendelea na kikao katika ukumbi wa halmashauri ya Msalala (Picha Sebastian Mnakaya)

Na Sebastian Mnakaya

Robo tatu ya Madiwani wa Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga limeazimia mbunge wa jimbo hilo Idd Kasimu kuitwa kwenye kamati ya maadili kwa madai ya kutokuhudhuria vikao vya baraza pamoja na kuwadhalilisha Madiwani hao wakati wa mikutano ya hadhara kwa wananchi.

Hayo yamesemwa na baadhi ya madiwani wa halmshauri hiyo, katika kikao cha kawaida baraza la madiwani, ambapo makamu mwenyekiti IBRAHIM SIX amesema kuwa kutokana na mwenendo wa mbunge huyo, baraza limeazimia aitwe kwenye kamati ya maadili ili kujibu madai hayo yanalalamikiwa na madiwani wa jimbo hilo la msalala.

Sauti ya makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Msalala Ibrahim Six
makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Msalala Ibrahim Six

Kwa upande wake diwani wa kata ya Segese JOSEPH MANYALA amesema kuwa kwa mujibu wa kanuni za baraza hilo mjumbe asipohudhuria vikao mara tatu mfululizo unaweza kujiondoa kuwa mjumbe, huku diwani wa Bulyanhulu SHIJA LUYOMBYA akisema kuwa kuitwa kwake ni kuthibitisha kauli zake katika mikutano ya hadhara.

Sauti ya diwani wa kata ya Segese Joseph Manyala na diwani wa Bulyanhulu Shija Luyombya

Nae afisa utumishi wa halmashauri ya Msalala Merry Nziku akifafanua kanuni za mjumbe kutohudhuria vikao vya baraza la madiwani, ambapo amesema kuwa wa mujibu wa kanuni jambo hilo halipaswi kujadili katika kikao cha baraza na badala yake lianzie kwenye kamati za maadili za halmashauri.

Sauti ya afisa utumishi wa halmashauri ya Msalala Merry Nziku

Halmashauri ya Msalala jumla ina madiwani 25 ambapo madiwani 21 wameedhimia mbunge huyo kuitwa kwenye kamati ya maadili kwa ajili ya kuhojiwa kwa kile wanachodai madiwani hao, huku madiwani 4 wakimuunga mkono mbunge kutokuitwa na kuhojiwa kwenye kamati hiyo.