Kahama FM
Kahama FM
May 2, 2025, 8:08 pm

Na Sebastian Mnakaya
Madiwani wa Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama Mkoani Shinyanga wametakiwa kuwahamasisha wananchi wao kujiandikisha katika zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura linaloanza leo nchini mzima.
Hayo yamesemwa na katibu tawala wa wilaya ya Kahama Glory Absalumu, katika kikao cha baraza la madiwani cha robo ya tatu, ambapo amesema kuwa kuelekea uchaguzi mkuu wananchi waliofikia umri wa miaka 18 kuandikishwa katika daftari hilo.
Aidha, ameongeza kuwa ili wawe na sifa za kupiga kura wanapaswa kujiandikisha katika dafatari la mpiga kura ili waweze kuchagua kioazi bora na wanayemtaka.
Naye, Diwani wa kata ya Ikinda Matrida Msoma amesema kuwa watatekeleza agizo hilo la kutoa elimu kwa wananchi wao ili waweze kujiandikisha na kupata kitambulisho cha mpiga, huku diwani wa kata ya Ngaya Kisusi Ilindilo akiwataka waliofikia umri wa miaka 18 kwenda kujiandikisha na wale ambao wamehama kutoka eneo moja kwenda nyingine kwa kubadilisha taarifa zao.

Kwa upande wake katibu mwenye wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Kahama Joachim Simbila amesema kuwa madiwani wanatakiwa kuendelea kutekeleza ilani ya Chama mpaka pale madiwani muda wao utaisha, huku akiwasiza kutoa elimu kwa wananchi ili kuwa na sifa za kupiga kura.
Zoezi la wananchi kujiandikisha katika maboresha la daftari la kudumu la mpiga kura limeanza leo nchi nzima na litakamili baada ya siku saba.