Kahama FM
Kahama FM
May 1, 2025, 10:23 pm

Na sebastian Mnakaya
Imeelezwa kuwa uchelewaji wa madawati yanayotolewa na mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu unaomilikiwa na kampuni ya Barrick katika Halmashauri ya Msalala umesababishwa na mwongozo wa utekelezaji wa mradi kubadilika.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo ROSE MANUMBA wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo kwenye kikao cha baraza la madiwani wa Halmashauri hiyo, ambapo amesema kuwa wanaendelea na utekelezaji wa kutengeneza madawani ili kuondokana changamoto hiyo.

Kwa upande wake, makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo Sixbeth Ibrahi akitoa taarifa juu ya ukamilishaji wa madawati hayo amesema mpaka sasa yanaendelea kutengenezwa ili kuondokana na changamoto hiyo ili wanafunzi wasikaye chini.
Nao, baadhi ya Madiwani akiwemo diwani wa kata ya Bugarama PRISCA MSOMA na diwani wa kata ya Bulyanhulu SHIJA LUYOMBYA wameomba hatua zichukuliwe ili kumaliza changamoto hizo huku wakiomba taarifa zitolewe kwa madiwani ili kila madawati yanapotolewa kuweka sawa takwimu.
