

April 1, 2025, 6:13 pm
”Majukumu makubwa ya idara ya udhibiti ubora wa shule ni kusimamia sheria, sera ya elimu, tararibu na miongozo inayotolewa na Wizara ya Elimu ili kuthibiti ubora wa shule zetu”
Na Sebastian Mnakaya
Mdhibiti mkuu wa ubora wa shule Halmashauri ya Manispaa ya Kahama Lazaro Michael Malili amezitaka shule za msingi na sekondari kufuata na kuzingatia sheria, sera ya elimu, taratibu na miongozo iliyotolewa na wizara ya elimu katika kutoa elimu bora na yenye viwango kuanzia kwenye miundombinu mpaka taaluma.
Malili ameyasema hayo wakati akizungumza katika kipindi cha Ukurasa Mpya kinachorushwa na Kahama fm, ambapo amesema wamekuwa na jukumu la kuzisimamia shule katika Manispaa ya Kahama kwa shule za msingi na Sekondari ili ziendelea kutoa elimu iliyobora, hasa kupita muundo mpya wa elimu ulioanza mwaka huu, ambapo wanafunzi kuishi darasa la 6 badala ya darasa la 7.