Kahama FM

Wasira: Wajumbe chagueni wagombea wanaokubalika kwa wananchi

March 28, 2025, 4:52 pm

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira (Picha na Sebastian Mnakaya)

”Utaratibu wa sasa katika kura za maoni CCM, wajumbe wameongezeka ili kuweza kupata viongozi wanaokubalika kwa wananchi”

Na Sebastian Mnakaya

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira amewataka wanachama wa chama hicho wanapoelekea katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika oktoba mwaka huu, kuwachagua wagombea wanaokubalika kwa wananchi ili kupata viongozi watakao shinda na kwenda kuwatumikia wananchi.

Wasira ametoa kauli hiyo wilayani Kahama mkoani Shinyanga katika ziara yake Kukagua Uhai wa Chama na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi wa Mwaka 2020-2025, ambapo amesema utaratibu wa sasa katika kura za maoni za chama cha mapinduzi CCM, wajumbe wameongezeka ili kuweza kupata viongozi wanaokubalika kwa wananchi.

Sauti ya Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira

Aidha wasira amewasisitiza wanachama kutokumchagua mgombea kwa sababu ya hali yake ya kifedha na badala yake wapokee na unapofika wakati wa kupiga kura wamchague kiongozi mwadilifu na anayekubalika kwa wananchi ili iwe kazi rahisi wakati wa kumnadi.

Sauti ya Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira

Kwa upande wao, baadhi ya wanachama wa CCM wilaya ya Kahama wakizungumza kwa nyakati tofauti, akiwemo Joseph Makwi na Edward Shimiliti wamesema kuwa watawachagua viongozi wanaokubalika katika jamii na wanaoweza kuwatumika wananchi vyema bila ya kusukumwa.

Sauti za wananchi wa Kahama Joseph Makwi na Edward Shimiliti
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa

Nae, mbunge wa jimbo la Ushetu Emmanuel Cherehani ameomba serikali katika halmashauri tatu za Kahama kuwepo na meneja TARURA ili kuweza kusimamia miradi ya maendeleo kikamilifu, huku mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akisema kuwa wameendelea kuwa na umoja katika utekelezaji miradi mbalimbali ya maendeleo.

Sauti ya mbunge wa jimbo la Ushetu Emmanuel Cherehani na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa