

March 27, 2025, 10:42 am
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira akizungumza na wanancha wa CCM mkoa wa Shinyanga
”Wajibu wa viongozi wa chama hicho ni kutatua shida za Wananchi hususani wa Bodaboda, Wanawake wajasiriamali na Wakulima, CCM sio chama cha msimu au uchaguzi, shabaha yetu ni kubadilisha maisha ya watu”
Na Sebastian Mnakaya
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira amewataka Viongozi wa chama hicho mkoa wa Shinyanga kutatua kero za Wananchi, ikiwa ni moja ya utekelezaji wa mkataba walioungia nao wakati wakiomba kura za kuongoza Serikali Mwaka 2020.
Wasira ametoa kauli hiyo mkoani Shinyanga katika ziara yake Kukagua Uhai wa Chama na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi wa Mwaka 2020-2025, amesema wajibu wa viongozi wa chama hicho ni kutatua shida za Wananchi hususani wa Bodaboda, Wanawake wajasiriamali na Wakulima.
Aidha Wasira amesema kuwa CCM ni chama kinachoangalia matatizo mbalimbali ya wananchi kwa lengo la kuzitatua wakiwemo wakina mama, wakulima na wasabirishaji (Boda boda) kwa amani na ulivu na si vinginevyo kwa baadhi wanavyodhani.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa, amemshukuru Rais Samia kwa kuutendea haki mkoa huo kwamba ametoa fedha nyingi na miradi ya maendeleo imetekelezwa.
Aidha, katika Mkutano huo Wasira alifanyiwa masuala ya kimila na kupewa jina la KilelaMhina likiwa na cheo cha Namhala Ntale.