Kahama FM

Wananchi watakiwa kuunga mkono ajenda za viongozi wa CHADEMA

March 27, 2025, 10:24 am

Mweyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Serengeti Jackson Mnyawami

Wananchi watakiwa kuunga mkono ajenda mbalimbali zinazoletwa na CHADEMA katika kuelekea Uchaguzi mkuu mwaka huu 2025

Na Sebastian Mnakaya

Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Kanda ya Serengeti kimewataka wananchi kuungana na Viongozi wa Chama hicho katika ajenda ambazo ni dira ya Chama hicho kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu 2025.

Wito huo umetolewa na Mweyekiti wa CHADEMA Kanda ya Serengeti Jackson Mnyawami wakati akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kumalizika kwa kikao cha ndani cha Viongozi wa Kanda hiyo kilichofanyika Wilayani Kahama na kwamba kampeni iliyo mbele yao imelenga kuhakikisha kunakuwa na usawa katika uchaguzi huo.

Aidha Mnyawami amesema kuwa wapo katika hatua ya kuwashirikisha wanachama ujumbe maalum kuhusu lengo la kutaka mabadiliko kwenye uchaguzi ili kuhakikisha viongozi wanaokubalika wanachaguliwa na kutangazwa kwa mujibu wa Katiba na sheria za nchi.

Sauti ya Mweyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Serengeti Jackson Mnyawami

Nae Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Kahama Mussa Bukango amesema lengo la kampeni iliyopo mbele yao ni kuhakikisha kunakuwa na uwiano wa wawakilishi kutoka kwenye vyama vyote ndani ya tume ili kuanikiza dhana ya haki na usawa huku akiwasihi wanachama wote kujitokeza kwenye mikutano yao.

Sauti ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Kahama Mussa Bukango

lengo la operesheni hiyo ni kuhakikisha kila mtu anapata haki kwa kuchaguliwa na katika kuzingatia uwiano wa wakikishi wa vyama ndani ya Tume ili kuleta usawa.