

March 25, 2025, 5:58 pm
Katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi oktoba mwaka huu 2025, vijana wengi wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika kushirik na kugombea nafai mbalimbali za uongozi
Na Sebastian Mnakaya
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinuzi (UVCCM) mkoani Shinyanga wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika oktoba mwaka huu 2025.
Wito huo umetolewa na mgeni rasmi ambaye ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Mabala Mlowa katika mkutano maalum wa baraza la vijana wa chama hicho (UVCCM), uliofanyika katika Manispaa ya Khama ambapo amewataka vijana kuchuka fomu ya uongozi ili kulisaidia taifa kwa kuwa wao ni damu changa.
Aidha Mlolwa amewataka vijana hao kuwa wasikate tamaa wakati wa kugombea ingawa machakato unakuwa mrefu na mgumu, huku akisisitiza juu ya kutokukihama chama inapotokea shindwa katika uchaguzi wa kura za maoni katika chama hicho.
Awali Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCC) mkoani Shinyanga Benard Werema, amemuomba mwenyekiti CCM mkoa wa Shinyanga vijana kupewa vipaumbele katika kugombea uchaguzi mkuu ili waweze kuwatumikia wananchi wakiwa na nguvu.
Kwa upande wao baadhi ya vijana wa chama Hicho wakizungumza kwa nyakati tofauti, akiwemo Britice Kagito na Mola Zabron wameshukuru viongozi wa chama hicho kwa kubariki wao kijitokeza kwa wingi ili waweze kugombea nafasi mbalimbali za uongozi, huku wakihitaji kuwa na vijana wenye sifa za kugombea.
Hata hivyo, Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Shinyanga katika kikao chao maalumu cha baraza hilo kimeazimia kumuunga mkono azimo la mkutano mkuu wa CCM la kuwapitisha wagombea wa uchaguzi mkuu 2025 katika nafasi ya Urasi na mgombea mwenza.