

March 22, 2025, 9:56 pm
”Wazazi na walezi wekezeni kwenye elimu kwa watoto wenu ili baadae waje kuwa wataalum katika sekta mbalimbali ”
Na Sebastian Mnakaya
Wazazi na walezi katika Halmashauri ya Ushetu Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kuwekeza kwenye elimu ya watoto wao ili kuandaa Watumishi bora wa baadaye watakaoisaidia jamii na taifa kwa ujumla.
Rai hiyo imetolewa na Mbunge wa Jimbo la Ushetu, Emmanuel Cherehani wakati akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa nyumba ya walimu (2 in 1) katika shule ya Sekondari Ngilimba iliyoo Kata ya Ulowa.
Cherehani amesema kuwa serikali itaendelea kuboresha katika sekta ya elimu ili kundelea kupata wataalum mbalimbi kutokea katika halmashauri ya Ushetu.
Awali akizungumza katika hafla hiyo Afisa elimu Sekondari wa Halmashauri hiyo, Mwl. Marwa Robert amesema kwa sasa changamoto inayowasumbua ni utoro wa wanafunzi na baadhi ya wazazi kutotoa ushirikiano kwa walimu katika suala laupatikanaji wa huduma ya chakula shuleni kwa ajili ya wanafunzi.
Uzinduzi huo pia uliambatana hafla ya kuwapokea Wanafunzi 142 wa kidato cha kwanza katika shule hiyo kwa mwaka 2025.