

March 17, 2025, 9:43 pm
Kulia ni Naibu Waziri wa TAMISEMI Zainab Katimba na katika ni Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya bunge TAMISEMI, Jastine Nyamoga (Picha na Sebastian Mnakaya)
kasi ya mkandarasi huyo haidhirishi ambapo mpaka sasa ametekeleza ujenzi kwa asilimia 48 pekee huku akiwa nje ya mkataba wa utekelezaji.
Na Sebastian Mnakaya
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imeiagiza serikali kutoongeza muda kwa kampuni ya SICHUAN ROAD AND BRIDGE (GROUP) CORPORATION L.T.D inayojenga barabara katika mradi wa uboreshaji Miji katika Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga baada ya kubainika kutekeleza mradi huo kwa kusuasua.
Akizungumza Mara baada ya kukagua barabara hizo Mwenyekiti wa Kamati ya TAMISEMI, Jastine Nyamoga amesema kasi ya mkandarasi huyo haidhirishi ambapo mpaka sasa ametekeleza ujenzi kwa asilimia 48 pekee huku akiwa nje ya mkataba wa utekelezaji.
Kwa Upande wake Naibu Waziri wa TAMISEMI, Zainab Katimba amesema Serikali itawafungia wakandarasi wanaoshindwa kutekeleza Miradi ambao rekodi zao zitaonesha ni wazembe na hawakamilishi miradi kwa wakati.
Awali akisoma taarifa ya Ujenzi wa Mradi huo Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI anayesimamia Miundombinu Mhandisi Rogatius Mativila amesema tayari wameshachukua hatua huku Mkandarasi huyo akitaja changamoto zinazomkabili.
Katika hatua nyingine, baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo akiwemo mbunge wa jimbo la Tarime vijiji Mwita Waitara na mbunge wa viti maalumu mkoa wa Shinyanga Salome Mkamba wametaka kujua wananchi wa kahama wananufaika vipi katika kufanyakazi ambazo haziitaji taaluma ili kujiongezea kipato.