Kahama FM

Marufuku kufukuzwa CCM Shinyanga bila ya kuzingatia kanuni

March 16, 2025, 4:41 pm

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa shinyanga Mabala Mlolwa (kulia) na Jumuiya ya Umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCC) mkoani Shinyanga Benard Werema (kushoto) picha na Sebastian Mnakaya

”Hakuna mwanachama yeyote kusimamishwa ama kufukuzwa kwenye chama bila ya kuzingatia taratibu na kanuni za chama”

Na Sebastian Mnakaya

Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga kimewataka viongozi mbalimbali wa chama hicho kusitisha kuwafunguza uwanachama na kuwasimisha katika nafasi mbalimabli bila kuzingatia taratibu na kanuni za chama ili kutenda haki kwa kila mmoja.

Agizo hilo limetolewa leo na mgeni rasmi ambaye ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Mabala Mlowa katika mkutano maalum wa baraza la vijana wa chama hicho (UVCCM), ambapo amesema kuelekea uchanguzi mkuu wanapawa kuwa makini katika maamuzi yao ya kufukuza uwanacha na badala yake wayaweke mezani na kudajili kwa pamoja ili kupata ufumbuzi.

Aidha Mabala amesema kuwa chama tayari kimetoa maelekezo kwa makatibu wote wa wilaya, kuwa kwa sasa hakuna mwanachama kusimamishwa ama kufukuzwa kiholela bila ya kuwa na vikao vya pamoja katika kufanya maamuzi.

Sauti ya mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Mabala Mlowa
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCC) mkoani Shinyanga Benard Werema (Picha na Sebastian Mnakaya)

Awali Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCC) mkoani Shinyanga Benard Werema, amesema kuwa kwa hivi karibu kumekuwa na changamoto wa vijana wa UVCCM wakifukuzwa na kusimamishwa uanachama pasipokuwa na kuzingatia kanuni za chama hicho.

Sauti ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCC) mkoani Shinyanga Benard Werema

Kwa upande wao baadhi wa wanachama wa chama hicho akiwemo Mola Zabron na Britice Kagito, wakizungumza na Kahama fm kwa nyakati tofauti wamemshukuru Mwenyekiti Mlolwa kwa kutoa msimamo wa chama kutofukuza watu bila ya kuzingatia taratibu na kanuni za chama.

Sauti ya baadhi wa wanachama wa chama hicho akiwemo Mola Zabron na Britice Kagito

Hata hivyo, Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Shinyanga katika kikao chao maalumu cha baraza hilo kimeazimia kumuunga mkono azimo la mkutano mkuu wa CCM la kuwapitisha wagombea wa uchaguzi mkuu 2025 katika nafasi ya Urasi na mgombea mwenza.