

February 5, 2025, 10:36 pm
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Ushetu, wilayani Kahama mkoani Shinyanga, limepitisha makadirio ya bajeti ya Shilingi bilioni 41.2 kwa mwaka wa fedha 2025/2026
Na Leokadia Andrew
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Ushetu, wilayani Kahama mkoani Shinyanga, limepitisha makadirio ya bajeti ya Shilingi bilioni 41.2 kwa mwaka wa fedha 2025/2026
Bajeti hiyo imeidhinishwa jana katika kikao cha Baraza la Madiwani cha halmashauri ya Ushetu, ambapo madiwani wamebainisha kuwa walijiwekea vipaumbele ikiwemo kuboresha vyanzo vya mapato, huku wakiipongeza serikali kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo ndani ya halmashauri hiyo
Akiwasilisha makadirio ya bajeti hiyo kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji wa halimashauri hiyo, Afisa Mipango, Shigela Ganja, amesema bajeti hiyo imeongezeka ikilinganishwa na ile ya mwaka 2024/25, ambayo ilikuwa Shilingi bilioni 35.5
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Nyamilangano, Robert Mihayo, amesema wamejipanga vizuri katika ukusanyaji wa mapato na kuthibiti utoroshaji wa mazao, huku akisisitiza wananchi wa ushetu kuhakikisha wanalipia ushuru ili kukuza uchumi wa halmashauri na taifa kwa ujumla