Wanachama CHADEMA Kahama wampongeza Lisu kwa ushindi
January 24, 2025, 10:59 am
Tundu Lisu ameibuka kuwa mshindi kwa nafasi ya mwenyekiti wa CHADEMA baada ya kupata kura 513 sawa na silimia 51.5% huku mpinzani wake wa karibu Freeman Mbowe 482 sawa na asilimia 48.3 na Odero Charles akipata kura 01%, katika uchaguzi uliofanyika January 21 2025
Na Sebastian Mnakaya
Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilayani Kahama mkoani Shinyanga wamekipongeza chama hicho kwa hatua walio ichukuwa ya kumchagua Tundu Lisu Kuwa mwenyekiti mpya wa chama hicho
Wakizungumza hayo mjini Kahama kwa nyakati tofauti baada ya Lisu kutangazwa kuwa mshindi kwa nafasi ya mwenyekiti Taifa, wamesema kuwa amechaguliwa katika kipindi cha wakati sahihi kwa mabadiliko ya chama hicho.
Kwa upande wake katibu mwenezi wa CHADEMA wilaya ya Kahama Mustafa Kiyege, amepongeza ushindi huo na kwamba kiongozi huyo mteule anapaswa kuendeleza mapambano ya kudai katiba mpya.