CCM Kahama watakiwa kuacha kampeni kabla ya muda
January 18, 2025, 6:21 pm
Baadhi ya viongozi wa chama hicho kuanza kufanya kampeni kabla ya muda wa kampeni kuanza
Na Sebastian Mnakaya
Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kuacha tabia ya kuanza kupiga kampeni kwa nafasi ya Ubunge na Diwani, kabla ya muda wa Uchaguzi pamoja na kupita katika majimbo ambayo ya viongozi.
Rai hiyo imetolewa na mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa, katika kikao cha mkutano mkuu ya jimbo la Ushetu, ambapo amesema kuwa atakayebainika atachukuliwa hatua za kinidhamu.
Aidha, katibu wa CCM wilaya ya Kahama Mfaume Kizibo amewataka viongozi kufanyakazi bila ya kusumbuliwa mpaka muda wao utakapotamatika.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita amesema kuwa wabunge wapo katika utekelezaji wa shughuli za kimaendeleo na kuwataka baadhi watu kuacha kuwaingilia katika ufanyajikazi wao mpaka uchaguzi utakapoanza.
Awali, akisoma taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya kipindi cha miaka 3, mbunge wa jimbo la Ushetu Emmanuel Chereahan amesema kuwa wamepokea fedha za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kiasi sha shilingi bili 190, huku baadhi wa wananchi wa Ushetu wameeleza kuchukizwa kwa baadhi ya watu kuanza kuingilia majukumu ya viongozi walioko madarakani.