Wakulima wa pamba Shinyanga wafundwa kilimo bora
September 30, 2024, 4:55 pm
Maafisa ugani katika kata 119 miongoni mwa kata 130 wamepatiwa pikipiki pamoja na vyombo vya kupimia ubora wa ardhi ili kuwafikia wakulima huku akiweka wazi kushuka kwa uzalishaji wa zao hilo katika mkoa wa Shinyanga.
Na Sebastian Mnakaya
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha amewataka wakulima wa zao la pamba mkoani humo kutolalamikia bei ya zao hilo bali kujikita katika kuzingatia namna bora na taratibu za ulimaji ili kuleta ongezeko la uzalishaji wenye tija na kujiinua kiuchumi.
Amesema hayo, wakati wa kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa iliyoketi kujadili masuala mbalimbali ndani ya mkoa huo, ambapo akieleza mikakati ya serikali kuiwezesha sekta ya kilimo katika maeneo mbalimbali mkoani humo.
Akizungumza nje ya kikao hicho mwakilishi wa wananchi jimbo la Kishapu Boniphace Butondo amesema jukumu la viongozi ni kuhakikisha elimu ya namna bora ya ulimaji wa zao hilo inawafikia wakulima.
Nao baadhi ya wakulima wa zao hilo kutoka mkoani Shinyanga Amosi mganga na Nicolaus Malembeka wameishukuru serikali kwa kutoa ruzuku na kuiomba kupanua soko la wanunuzi ili waweze kuuza kwa bei nzuri zaidi