Wananchi kata ya Nyahanga waomba kujengewa shule ya sekondari
July 15, 2024, 3:40 pm
wameimarisha ulinzi katika maeneo hatarishi kwa kuweka ulinzi wa jeshi la jadi katika nyakati za asubuhi pindi wanafunzi wanapokwenda shuleni.
Na Sebastian Mnakaya
Baadhi ya wananchi wa kata ya Nyahanga Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga wameiomba serikali kujenga shule nyingine ya sekondari ili kuondokana na vitendo vya uhalifu kwa wanafunzi wanavyofanyiwa wakati wa kwenda shule nyakati za alhifajili kutokana na umbali wa sekondari ya sasa.
Akizungumza na kahama fm Anjella Mwandu mkazi wa mtaa wa nyahanga wamesema kijana wake amekutana na vikaba wakampora sare zake za shule, viatu na begi huku mwanafunzi Emmanuel Mabula aliyefanyiwa kitendo hicho akielezea tukio hilo.
Baadhi ya wananchi wa kata hiyo wakizungumza kwa nyakati tofauti wamesema wanashukuru kujengwa kwa shule ya sekondari ya kata ya sasa, huku wakiomba serikali kuongeza shule nyingine kutokana na kata hiyo kuwa na eneo kubwa.
Nae, diwani wa kata ya Nyahanga Pancreas Ikongoli, amesema baada ya tukio hilo wameimarisha ulinzi katika maeneo hatarishi kwa kuweka ulinzi wa jeshi la jadi katika nyakati za asubuhi pindi wanafunzi wanapokwenda shuleni.