Watoto wanaoishi mazingira magumu wawekewe mazingira wezeshi wapate elimu
June 14, 2024, 3:56 pm
halmashauri hiyo ilikuwa imetenga fungu ili kuwasaida watoto na baadae kilifutwa kutokana na serikali kuanzisha elimu bure
Na leokadia Andrew
Walimu wa shule za msingi na sekondari halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga wameiomba serikali kuwasaidia na kuwatengenezea mazingira mazuri watoto wanaoishi katika mazingira magumu ili waweze kusoma na kupata elimu itakayowasaidia katika maisha yao.
Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa umoja wa walimu wa shule za msingi Msalala Daudi Mussa na mwalimu Zacharia Mganga na katika kikao cha wadau wa elimu kilichofanyika katika halmashauri hiyo.
Wameiomba serikali kujenga shule maalumu kwa ajili ya watoto hao wanaoishi katika mazingira magumu na kuunda mfuko maaluma wa kuwasaidia kupata elimu ili waweze kutumiza malengo hayo.
Naye, mtendaji wa kata ya Segese katika halmashauri hiyo Partick Mahona amesema baadhi ya wanafunzi wanamaliza kidato cha nne na wanafanya vizuri, huku wakikosa fursa ya kuendelea na masomo kutokana na kukosa fedha na kuomba halmashuri hiyo kuwasaidia watoto hao.
Kwa upande wake kaimu mwenyekiti wa halamshauri hiyo Frola Sagasaga akifafanua juu ya suala hilo amesema awali halmashauri hiyo ilikuwa imetenga fungu ili kuwasaida watoto na baadae kilifutwa kutokana na serikali kuanzisha elimu bure na kuwaomba wadau wa maendelea kupita baraza la madiwani kuona manna ya kuwasaidia.