Kahama FM

Wawekezaji toeni fursa za ajira kwa vijana wazawa

June 5, 2024, 5:07 pm

Mkuu wa wilaya Kahama Mboni Mhita(wa pili kulia) akikagua ujenzi unaoendelea katika mgodi wa dhababu Super Mwabomba(picha na Sebastian Mnakaya)

 wawekezaji endeleeni  kuwapa kipaumbele wazawa wa maeneo husika kwa kuwapatia kazi ambazo wanaziweza kuzifanya ili nao wapate kipato kupitia uwekaziji huo.

Na sebastian Mnakaya

Mkuu wa Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga Mboni Mhita amewataka wawekezaji katika sekta ya madini kutoa ajira na fursa kwa wananchi wazawa katika maeneo yanayozungukwa na migodi ili wote kwa pamoja wanufaike na uwekezaji huo.

Mhita ameyasema hayo wakati akikagua ujenzi unaoendelea katika mgoni wa dhababu Super Mwabomba uliyopo kata ya Idahina Halmashauri ya Ushetu, ambapo amewataka wawekezaji hao kuendelea kuwapa kipaumbele wazawa wa maeneo hayo kwa kuwapatia kazi ambazo wanaziweza kuzifanya ili nao wapate kipato kupitia uwekaziji huo.

sauti ya mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita

Kwa upande wake, mwenyekiti wa mgodi wa dhahabu wa Super Mwabomba Finias Kanani, amesema kwa kipindi cha miaka 9 iliyopita hali ya uhalifu ilikuwepo katika maeneo hayo na kuomba kamati ya ulinzi na usalama kulishughulikia ili kuwe na usalama wa kutosha kabla ya kuanza uzalishwaji katika mgodi huo.

sauti ya mwenyekiti wa mgodi wa dhahabu wa Super Mwabomba Finias Kanani

Naye, afisa madini mkoa wa kimadini Kahama Joseph Kumburu, amewataka wamiliki wa mgodi huyo ujenga ukuta kwa ajili ya usalama pamoja na kuweka mitambo kwenye eneo moja, huku mkaguzi wa jeshi la zima moto wilaya ya Kahama Stanley Luhwago akiwataka kuzingatia kikamilifu suala la usalama pamoja na kukamilisha baadhi ya vitu kabla ya uzalishaji.

Afisa madini mkoa wa kimadini Kahama Joseph Kumburu