Zaidi ya bil. 44 kutumika mradi wa maji ya ziwa Victoria Ushetu
June 3, 2024, 7:45 pm
Changamoto ya barabara pamoja na ujenzi wa kituo cha afya kwenye kata hii kama Wizara ya Fedha tumelipokea tutakwenda kulifanyia kazi mara baada ya kukamilika kwa mradi huu, niwasihi wananchi tukawe walinzi wa miundombinu hii ili ikawe na manufaa na kuduma kwa muda mrefu.
Na Sebastian Mnakaya
Waziri wa fedha Dkt. Mwigulu Nchemba amewahakikishia wananchi wa halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga kuwa imetenga kiasi shilingi bilioni 44 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi mkubwa wa maji ziwa Victoria na mchakato wote wa fedha umekamilika huku mradi huo hautachuka muda mrefu kukamilika.
Waziri Nchemba ameyasema hayo jana katika hafla ya kutia saini mradi wa maji ziwa Victoria kutoka Kahama kwenda halmashauri ya Ushetu, ambapo amesema kuwa viongozi hawatakiwi kuwa na vikwazo katika kutekeleza na kukamilisha mradi huo utakaochukua miezi 24 kukamilika kwake.
Kwa upande wake Waziri wa Maji Juma Aweso amesema mkandarasi anayetekeleza mradi huo akamilishe kwa wakati ili wananchi wasiendelee kuteseka kutokana na kukosa maji safi na salama kwa muda mrefu pamoja na kuwataka viongozi ngazi ya wilaya na mkoa kuwachukulia hatua kwa wale watakaobainika kukwamisha mradi huo.
Naye, mbunge wa jimbo la ushetu Emmanuel Cherehani katika halfa hiyo amewashukuru viongozi mbalimbali walioshiriki pamoja na kuhakikisha mchakato wa maji ya ziwa Victoria unakamilika mpaka kufikia hatua ya kutia saini
Hata hivyo, utekelezaji wa mradi huo utahusisha ujenzi wa wa matenki matatu yenye ujazo wa lita 500,000, 300,000 na 100,000 katika maeneo tofauti kata ya ulowapamoja na bomba kuu aina ya chuma lenye kipenyo cha kuanzia milimita 350 hadi milimita 100 lenye uwezo wa kilometa 76 kutoka katika manspaa ya kahama kwenda ulowa hadi kwenye matanki hayo.