Wananchi watakiwa kuhifadhi chakula
May 27, 2024, 11:11 pm
Wafanyabiashara wengi wamekuwa wakinunua mazao kwa bei ya chini hali inayosababisha wakulima kuuza chakula na kusahau kukihifadhi ya ajili ya msimu ujao.
na Sebastian Mnakaya
Wananchi wa halmashauri ya ushetu wilayani kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kuendelea kuhifadhi chakula ili kuepuka upungufu wa chakula kwa msimu ujao kutokana na mvua zisizokuwa na uhakika.
Wito huo umetolewa na afisa kilimo wa Halmashauri ya Ushetu MAPENZI MSHANA ambapo amesema kuwa wafanyabiashara wengi wamekuwa wakinunua mazao kwa bei ya chini hali inayosababisha wakulima kuuza chakula na kusahau kukihifadhi ya ajili ya msimu ujao
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya Ushetu GAGI LALA amewaomba maafisa kilimo kutoa elimu kwa wakulima namna bora ya kuvuna pamoja na kutunza mazao yao yawe salama kutokana na kuvuna mazao kwa wingi
Naye, diwani wa kata ya Nyamilangano ROBART MIHAYO amesema kuwa katika kipindi hiki wakulima hawapaswi kuuza chakula na badala yake wakitunze kwa ajili ya familia zao.