Kahama FM

Nyumba 11 zabomoka kutokana na mvua kubwa,Kijiji cha Mwashimbai

May 1, 2024, 4:36 pm

Mkuu wa wilaya ya Kahama mhe.Mboni Mhita akiwasalimia waathirika wa mvua (picha na Sebastian Mnakaya)

Nyumba zilizoanguka hazikuzingatia ujenzi bora wenye kuvumilia hali ya hewa ya sasa

Na Sebastian Mnakaya

Zaidi ya nyumba 11 katika kijiji cha Mwashimbai kata ya Ngaya halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga zimeanguka kutokana na changamoto ya mvua zinazoendelea kunyesha, huku zilizoarithika ni zile zilizojengwa kwa kutumia udongo

Mkuu wa wilaya ya Kahama MBONI MHITA, amezitembelea kaya zilizoathirika kwa ajili ya kutoa msaada na kuwafariji waathirika ambapo amesema nyumba zilizoanguka hazikuzingatia ujenzi bora wenye kuvumilia hali ya hewa ya sasa

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita

Nae, mwenyekiti wa kijiji cha Mwashimbai PAKI NTEMI amesema baada ya mvua kutika maji yaliendelea kujaa na kusababisha nyumba nyingi kuanguka, huku mzee BUKWELE KULUNGA aliyeathirika na mvua hizo mwenye watoto 30 na wajukuu 30 ameiiomba serikali msaada wa chakula na mahali pa kuishi kutokana na nyumba yake kuanguka.

Sauti ya mwenyekiti na mwananchi

Kwa upande wake diwani wa kata ya Ngaya, KISUSI ILINDILO amesema mpaka sasa watu zaidi ya 200 pamoja na kupoteza chakula na makazi ya kuishi, huku kwa hatua za awali wamewahifadhi kwenye mashule na nyumba ambazo zina nafasi ya kuishi wengine wakihifadhiwa na ndugu zao.

Sauti ya diwani wa kata ya Ngaya kisusi Ilindilo