KAHAMA:Wanafunzi wakike shule ya sekondari Mapamba waiomba serikali iwapelekee walimu wa kike.
December 9, 2021, 4:20 pm
Wanafunzi wakike katika shule ya sekondari Mapamba Halmashuri ya ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga wameiomba serikali iwapelekee walimu wakike ili waweze kuhudumia pindi wanapohitaji msaada maalum katika masuala ya wanawake.
Hayo yamesemwa na wanafunzi wa shule ya sekondari mapamba katika mkutano wa mbunge wa jimbo ushetu EMMENUEL CHARAHANI akiwa na wananchi na wanafunzi hao wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa madarasa katika shule hiyo, ambapo wameiomba serikali kutatua changamoto hiyo ili inayowakabili tangu kuanzishwa kwa shule hiyo.
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la ushetu EMMANUEL CHARAHANI amesema kuwa anashughulikia changamoto hiyo,huku akiwataka maafisa elimu wa halmashauri hiyo kutembelea shule zote za sekondari na msingi ili kubaini changamoto mbalimbali zinazo wakabili walimu na wanafuzi.
Nae, Diwani wa kata ya mapamba YOHANA MANGE amesema kuwa tatizo hilo tayari amelifikisha kwenye baraza la madiwani na kuomba serikali ili kuweza kuwasaidia wanafunzi wa kike katika shule hiyo
Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Mapamba LAU JOHN SINGASINGA amesema shule hiyo ilianzishwa mwaka 2019 na bado inachangamoto ya miundo mbinu na kuwaomba wadau wa maendeleo na serikali kuendelea kuchangia ili kupunguza changamoto zinazoikabili. I
Hivi karibuni shule ya sekondari mapamba imesajiliwa kuwa shule rasmi ambapo awali ilikuwa shule shikizi ya kisuke, na hadi sasa ina wanafunzi Zaidi ya 150 kwa kidato cha kwanza hadi cha tatu.