Kahama:Mbunge wa Kahama mjini achangia ujenzi wa shule ya Sekondari Malunga.
September 27, 2021, 6:50 pm
Mbunge wa jimbo la Kahama Mjini JUMANNE KISHIMBA amechangia millioni moja na laki moja kwa ajili ya kukunua matofali ya kukamilisha ujenzi wa sekondari ya Kata ya Malunga wilayani Kahama Mkoani Shinyanga iliyoanza kujengwa hivi karibuni.
Akizungumza katika ziara yake ya kukagua ujenzi wa shule hiyo ya sekondari, KISHIMBA amesema jitihada zilizopo ni kuhakikisha madarasa tisa yanayojengwa na kumalizika mapema ili kufikia mwezi January 2022 wanafunzi waanze kusoma katika shule hiyo.
Amesema kila sehemu anapita na kuchangia michango ya kukamilisha ujenzi wa shule pamoja na miundombinu mbalimbali ambapo katika shule ya msingi Malunga amechangia shilingi Laki mbili kwa ajili ya umeme na vyoo vya walimu ambavyo vimekua changamoto.
Kwa upande wake Mtendaji wa Kata ya Malunga, EMANUEL MLOSO amesema wananchi wanatakiwa kuendelea kujitoa kuchangia ujenzi wa Maboma na wakikamilisha wataiomba halmashauri imalizie maboma hayo.
Ujenzi wa shule hiyo ya sekondari Malunga umeanzishwa na wananchi wa Kata hiyo kwa kuchangia michango mbalimbali pamoja na ujenzi wa maboma.