Ukatili wa kijinsia wapungua baada ya wananchi kuelimishwa.
August 18, 2021, 8:58 pm
Imeelezwa kuwa katika Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga, ukatili wa kijinsia umepungua baada ya wananchi kuelimishwa kupitia mikutano ya Kijiji, ikiwemo wanandoa kutelekeza familia na wanafunzi kuachishwa shule.
Akizungumza na Kahama FM Afisa Tarafa ya Dakama TUMSHUKURU MDUI amesema kuwa katika halmashauri hiyo ukatili umepungua kwa sababu ya Serikali imeweka mikakati ya kutoa elimu pamoja na kuwaonesha wananchi ni wapi pa kupeleka malalamiko na kesi zao zinazohusu ukatili wa kijinsia katika jamii.
Hata hivyo, MDUHI amesema katika ofisi za watendaji wa vitongoji na kata pamoja na ofisi za vijiji wanashughulikia ukatili wa kijinsi kwa kushirikiana na wananchi ili kuondokana na hali ya wanafunzi kutokwenda shule kwa ajili ya uchungaji na wanandoa kutelekeza kwa wanafamilia zao.
Naye diwani wa kata ya Igunda TABIA KATOTO amesema kuwa baada ya wananchi wa kata hiyo kupata msaada wa kisheria imesaidia kupunguza ukatili wa kijinsia kwa wanawake na wanaume.
Katika Halmashauri ya Ushetu, kwa siku za hivi karibuni ukatili wa kijinsia umepungua ikilinganishwa na miaka mitano ya awali kutokana na elimu kuendelea kutolewa.