wilaya ya Kahama imeombwa kuangalia upya utaratibu katika zuio la uuzwaji wa nishati ya mafuta majumbani.
August 18, 2021, 8:51 pm
Madiwani wa Halmashauri ya ushetu wilayani Kahama mkoani shinyanga wameiomba halmashauri hiyo kuangalia upya utaratibu katika zuio la uuzwaji wa nishati ya mafuta majumbani kutokana na kuwa na vituo vichache katika halmashauri hiyo yenye kata 20.
Wakizungumza katika mkutano wa baraza la madiwani robo ya nne, wamesema kuwa zuio hilo litasababisha wananchi wenye vyombo vya moto kuhifadhi majumbani ambapo itakuwa ni hatari.
I
Kwa upande wake kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya ushetu DEUS KAKULIMA, amesema kuwa zuio hilo ni la nchi nzima, na wafanyabiashara wanapaswa kutii agizo hilo kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA)
Hata hivyo, agizo hilo limetolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) baada ya kuwepo uuzwaji wa nishati ya mafuta ya petrol na dizeli kwenye mitaa na vijiji pasipo kufuata taratibu na kanuni, pamoja na namna ya kujikinga na majanga ya moto yanapotokea.