Mkazi wa Nyasubi wilayani Kahama leo afikishwa katika Mahakama ya wilaya.
April 21, 2021, 7:15 pm
Mkazi wa Nyasubi wilayani Kahama mkoani Shinyanga JONATHANI JULIUS MANYAMA mzanaki (32) leo amefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Kahama kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa kwa shauri lake la ubakaji Pamoja na kumpa ujauzito mwanafunzi wa kidato cha nne wa shule ya sekondari Nyasubi .
Mbele ya Hakimu mkazi wa mahakama hiyo DAVID MSALILWA mwendesha mashtaka upande wa Jamuhuri ATHUMANI KISANGO amesema mnamo January 22 mwaka huu,eneo la Nyasubi mshtakiwa alimbaka msichana (17)katika shamba la mahindi lililopo eneo hilo ambapo muhanga wa tukio alikuwa akipita.
KISANGO amesema mshitakiwa alimbaka mwanafunzi huyo (17) wa kidato cha nne ambapo ni kinyume cha sheria kifungu cha 130(1) na (2) ,(e) na kifungu cha 131(1) cha sheria cha kanuni ya adhabu.
baada ya kusomewa maelezo ya awali amekubali majina na anuani yake ya makazi lakini amekana kumbaka mlalamikaji, huku upande wa jamuhuri ukiongozwa na mwendesha mashtaka athumani kisango umesema utaleta mashahidi wanne may 12 mwaka huu kesi itakapoanza kusikilizwa tena ambapo mshitakiwa anaendelea na dhamana yake.