FM Manyara

Afariki baada ya kubakwa na kutobolewa jicho, Sillo alaani

7 October 2024, 8:34 pm

Serikali yalaani tukio la mwanamke aliyebakwa na kulawitiwa  mkoani Manyara ambapo  jamii  imetakiwa kukemea vitendo hivyo vya kikatili nakuwalea watoto wao  katika maadili mazuri.

Na Mzidalfa Zaid

Mwanamke mmoja wa kata ya Magugu mkoani Manyara amefariki baada ya kubakwa  na kulawitiwa na vijana pamoja na kumtoboa jicho moja.

Akizungumza na FM Manyara diwani wa viti maalum tarafa Mbugwe Naomi Richard amesema baada ya tukio hilo juhudi alizozifanya ni kuhakikisha vijana waliofanya tukio hilo wanakamatwa.

Sauti ya diwani wa viti maalumu tarafa Mbugwe Naomi Richard

Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Matufa Ramadhani Mangi amesema matukio ya ukatili yameshamiri katika kata hiyo na yanasababishwa na wanachi kushindwa kutoa ushirikiano.

Sauti ya mwenyekiti wa kijiji cha Matufa Ramadhani Mangi

Aidha,naibu waziri wa mambo ya ndani ambae pia ni mbunge wa jimbo la Babati vijijni Daniel Silo amelaani tukio la mwanamke huyo na ameitaka jamii kukemea vitendo hivyo vya kikatili na kuitaka jamii kuwalea watoto wao  katika maadili mazuri.

sauti ya naibu waziri wa mambo ya ndani ambae pia ni mbunge wa jimbo la Babati vijijni Daniel Silo