FM Manyara

Mati Super Brand Ltd yatoa zawadi kwa wateja wake

12 October 2024, 9:07 pm

Picha ya Mkurugenzi wa kampuni ya uzalishaji vinywaji changamshi ya  Mati Super Brand ltd David Mulokozi

Wakati wiki ya huduma kwa wateja ikiwa imehitimishwa ,kampuni ya uzalishaji vinywaji changamshi ya  Mati Super Brand ltd imegawa zawadi mbalimbali kwa wateja wao.

Na Mzidalfa Zaid

Mkurugenzi wa kampuni ya uzalishaji vinywaji changamshi ya  Mati Super Brand ltd David Mulokozi amesema wamehitimisha wiki ya huduma kwa wateja kwa kupunguza bei  pamoja na kugawa zawadi kwa wateja wake .

Mulokozi amesema wamefanya hivyo kutokana na wateja hao kununua bidhaa zinazozalishwa na kampuni hiyo hali ambayo itawapa motisha ya kuendelea kununua bidhaa hizo.

Amesema mbali na vinywaji changamshi wana mkakati wa kutengeneza vinywaji laini ikiwemo maji na juice ambapo amewataka wananchi kuendelea kuvuta subira hadi pale vitakapoweviweka sokoni.

sauti ya Mkurugenzi wa kampuni ya uzalishaji vinywaji changamshi ya  Mati Super Brand ltd David Mulokozi

Katika hatua nyingine amewataka wananchi mkoani Manyara kuendelea kujiandikisha katika daftari la mkazi ambalo limeanza octoba 11, 2024 hadi octoba 20 mwaka huu.

Katika hatua nyingine amewataka wananchi mkoani Manyara kuendelea kujiandikisha katika daftari la mkazi ambalo limeanza octoba 11, 2024 hadi octoba 20 mwaka huu.