Adhana FM

Watu wenye ulemavu wa uziwi ni miongoni makundi yanayoishi kwenye dimbwi la umasikini Zanzibar

29 September 2021, 7:36 pm

Na mwandishi wetu, Wilaya Kusini Unguja.

Jumuiya Ya Viziwi Zanzibar Imesema  Kundi Kubwa La  Watu Wenye Ulemavu Wa   Uziwi Liko Nyuma   Kimaendeleo Hususan  Vijijini.

Mwenyekiti Wa Jumuiya  Viziwi Zanzibar  Bi Asha Ali Haji  Ameyaeleza  Hayo Mara  Baada Ya  Kufanya  Kazi  Za  Usafi  Katika Hospitali Ya Wilaya  Makunduchi  Na  Kazi Ya Utandazaji Wa Kifusi  Katika Soko Jipya La  Kijini Makunduchi Ikiwa  Shamra Shamra Ya Kuelekea  Kwenye Kilele Cha Maadhimisho Ya  Wiki Ya Viziwi Duniani.

Amesema Licha  Ya Serekali Na  Taasisi Mbali Mbali Nchini  Kuendelea  Na Juhudi Za  Kuwakomboa Watu Wenye  Ulemavu Wa  Uziwi  Bado Jamii  Haina  Muamko Wa  Kutosha Katika  Kutetea  Haki Zao  Hivyo  Amewashauri  Wazazi  Na Walezi  Kuacha Tabia Ya Kuwaficha  Watoto Wao  Na Badala Yake Kuwashirikisha Katika Masuala  Ya Kijamii  Ikiwemo Kuwapatia Elimu Ya Lugha Za Alama .

Nae Kijana Mwenye Ulemavu Wa Uziwi  Abdul Aziz  Muhammed Mahfoudh Amesema Wakati Umefika Sasa Serekali Na  Jamii Kuona  Umuhimu Wa  Kulipa Kipau Mbele Suala La Kujifunza Lugha Ya  Alama  Kwa  Lengo La Kurahisisha  Upatikanaji  Wa Mawasiliano   Ili  Waweze  Kuzifikia Fursa  Mbali  Mbali Nchini.

Akizungumza  Kwa Niaba Ya  Daktari Dhamana  Wa Hospitali Ya Wilaya Makunduchi  Daktari  Amour Muhsin Burhan  Ameishukuru Jumuiya Hiyo Kwa Hatua  Yakeyakufanya Usafi Hospitalini Hapo Na  Kuwataka  Kuendelea  Kushiriki Kikamilifu  Katika Kazi Zinazohusiana Na  Jamii Huku Akiiomba  Jamii Kuthamini Juhudi Zao.

Wiki Ya Viziwi Husherehekewa  Kila Mwaka Ifikapo   Wiki Ya Mwisho Ya  Mwezi Wa Septemba Na Kauli Mbiu Kwa Mwaka Huu Ni  Sherehekea Ustawi Wa Jamii  Ya Watu Wenye Ulemavu Kwa Maeneo Makuu Ya  Lugha Ya Alama Na Tambua Uwepo Wa Historia Nzuri Ya Kupendeza  Ya Watu Wenye Ulemavu Wa Uziwi .