

12 March 2025, 12:41 pm
Wananchi wametakiwa kuimarisha usafi na kujikinga na magonjwa ya mlipuko kama marburg katika maeneo yao.
Na Abdunuru Shafii
Wakazi wa mtaa wa Mjimwema kata ya Nguruka halmashauri ya wilaya Uvinza wameeleza namna wanavyojikinga na magonjwa ya mlipuko ikiwemo ugonjwa wa marburg.
Wamesema hayo wakizungumza na Uvinza FM ilipowatembelea na kuhitaji kufahamu wananchi wanajikinga vipi na ugonjwa wa marburg.
Ili kuhakikisha jamii inakuwa salama dhidi ya magonjwa ya mlipuko, viongozi wa eneo hilo nao wameweka mikakati maalum.
Mwenyekiti wa kitongoji cha Bweru Kusini Masumbuko Swedi ameeleza mikakati hiyo ya kuimarisha usafi na kujikinga na magonjwa ya mlipuko katika maeneo yake.
Naye Mratibu wa Afya Mulla Mnyanyi ameeleza namna wananchi wanavyoweza kujikinga na magojwa ya mlipuko hasa ugonjwa wa marburg ambapo wanatakiwa kuacha kula nyama ya wanyama wa mwituni wakiwemo nyani, sokwe na popo.